Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kutoa amri ya kukamatwa na kupigwa na wengine kuuawa kwa waandamanaji waliokuwa wanapinga utawala wake mnamo mwaka wa 2012.
Mahakama katika jiji la Cairo nchini Misri i metoa hukumu hiyo kwa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani mnamo mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake yaliyokuwa yakifanyika sehemu mbalimbali nchini humo.
Watuhumiwa wengine 14 nao waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka kama ya Morsi nao wamehukumiwa kwenda jela miaka 20 kila mmoja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni