Juventus imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo dhidi ya wageni wao Monaco, baada ya kuwafunga bao 1-0.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Arturo Vidal kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 57 ya kipindi cha pili cha mchezo huo. Matokeo hayo yamewaweka pazuri Juventus kusonga mbele, kwani katika mchezo wa marudiano wanatakiwa kupata sare au ushindi wowote ili kuweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali.
Wachezaji wa Juventus wakishangilia mbele ya mashabiki wao baada ya Vidal kufunga goli pekee katika dakika ya 57 kwa njia ya penati.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni