Wakicheza nyumbani, Porto walijipatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya mlinda mlango wa Bayern Munich, Manuel Neuer kumuangusha katika eneo la hatari mshambuliaji Jackson Martinez, ambapo mwamuzi wa mchezo huo Carlos Velasco Carballo aliipa Porto penati iliyofungwa na Ricardo Quaresma.
Kwa matokeo hayo, Porto wamejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, kwani katika mchezo wa marudiano Allianz Arena, watatakiwa kutokubali kufungwa zaidi ya mabao 3-0, au walazimishe sare ya aina yeyote ile.








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni