.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Aprili 2015

TIKETI ZA PAMBANO LA FLOYD MAYWEATHER NA MANNY PACQUIAO ZAANZA KUUZWA

Bondia Floyd Mayweather ( kushoto ) akijifua na Uncle Roger kabla ya pamabano lake.
Bondia Manny Pacquiao ( kulia ) akijifua chini ya mkufunzi wake Freddie Roach kabla ya pambano lake. 

Hatimaye tiketi kwa ajili ya mashabiki watakaotaka kwenda kushuhudia pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa kote ulimwenguni kati ya mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao zimeanza kuuzwa toka jana jumatano. 

Zaidi ya tiketi 1000 zitauzwa kwa kati ya dola za kimarekani 1,500 hadi dola 7,500 kwa tiketi moja. 

Ukumbi wa MGM Grand Arena ambako pambano hilo ndipo litakapofanyika May 02'2015 unauwezo wa kuchukua watazamaji 16,500. 

Hata hivyo nyingi ya tiketi hizo zinatarajiwa kuuzwa kwa kambi mbili tofauti zinazowaunga mkono mabondia hawa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni