Tume ya Uchaguzi (NEC) imesema
haitoweza kuendelea na zoezi la kura ya maoni kama ilivyopangwa
kufanyika Aprili 30, kutokana na kutokamilika kwa zoezi la uboreshaji
daftari la kudumu la wapigakura.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa zoezi
lolote la kupiga kura likiwepo la kura ya maoni ya Katiba
inayopendekezwa linategemea kuwepo kwanza kwa daftari la kudumu la
wapigakura.
Licha ya kutangaza kuhairishwa
zoezi la upigaji kura ya maoni hadi baadae, Jaji Lubuva amesema zoezi
la uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litaendelea katika
mikoa ya Lindi, Ruvuma, Iringa na Mtwara.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni