Zaidi ya wahamiaji 400 toka Afrika waliokuwa wakijaribu kuingia barani Ulaya wanahofiwa kuwa wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama walipokuwa wakitokea nchini Libya kuelekea Ulaya.
Inaripotiwa kuwa zaidi ya wahamiaji 8,000 walikuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean mwishoni mwa wiki.
Boti hiyo iliyozama ilikuwa na wahamiaji 550, na ilizama saa 24 baada ya kuondoka pwani ya Libya.
Manusura 150 waliokolewa na kukabidhiwa katika mamlaka husika nchini Italia.
Mfanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu akiwa amembeba mtoto mchanga wa mmoja wa wahamiaji huku akiwa amefunikwa kwa blanketi kumuepusha na baridi kali baada ya kupokelewa katika kisiwa cha Cicilian
Baadhi ya wahamiaji wakiwa katika boti
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)







Hakuna maoni :
Chapisha Maoni