Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakichukua picha kutoka moja ya magari ya wagonjwa lililobeba miili ya wauza dawa za kulevya raia wa Australia, Myuran Sukumaran na Andrew Chan baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya kupatikana na hatia.
Serikali ya Indonesia imetekeleza hukumu ya kuuawa kwa kupigwa risasi hadi kufa wasafirishaji nane wa dawa za kulevya baada ya kupatikana na hatia ya kuingiza dawa hizo nchini humo hivyo kuhukumiwa adhabu ya kifo licha ya mataifa mbalimbali ulimwenguni kuitaka Indonesia kutotimiza adhabu hiyo.
Hata hivyo Rais wa nchi hiyo, Joko Widodo amechelewesha kuuawa kwa mfungwa wa tisa ambaye ni raia wa Ufilipino, Mary Jane Veloso baada ya mwanamke mmoja kujitokeza na kujisalimisha polisi nchini Philipines akisema yeye ndiye aliyemuhadaa Mary kubeba dawa za kulevya na kupeleka nchini Indonesia ambako alikamatwa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni