.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Aprili 2015

MABONDIA MANNY PACQUIAO NA FLOYD MAYWEATHER WAWASILI LAS VEGAS KWA MBWEMBWE

Bondia Floyd Floyd Mayweather ( mbele ) akiwa ameongozana na promota wake Leonard Ellerbe wakiingia katika ukumbi wa MGM Grand  hapo jana, ikiwa ni siku moja tu baada ya mpinzani wake Manny Pacquiao kuwasili Las Vegas tayari kwa pambano lao siku ya jumamosi.
Bondia Floyd Mayweather akizungumzia pambano lake lijalo na mpinzani wake Manny Pacquiao siku ya jumamosi.
MNAUONA MSULI!! Bondia Manny Pacquiao akiwasalimia mashabiki wake mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Mandalay Bay mjini Las Vegas akitokea Los Angeles alikokuwa ameweka kambi akijifua tayari kwa pambano lake na Floyd Mayweather siku ya jumamosi.
Mabondia, Floyd Mayweather ( kushoto ) na Manny Pacquiao walipotambulishwa kwa waandishi wa habari. 

Homa ya pambano la ngumi la aina yake linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mamilioni ya mashabiki wa mchezo huo kote ulimwenguni imezidi kupamba moto baada ya mabondia wote wawili, Floyd Mayweather na mpinzani wake Manny Pacquiao kuwasili mjini Las Vegas. 

Wa kwanza kuwasili katika mji huo alikuwa Manny Pacquiao aliyefikia katika hotel ya Mandalay Bay akiwa na msafara mkubwa. 

Pacquiao alisafiri umbali wa maili 270 kutoka Los Angeles kwa basi maalum hadi Las Vegas ambako pambano hilo ndipo litakapofanyika jumamosi. 

Pacquiao raia wa Ufilipino alipokelewa na mamia ya mashabiki na nyimbo zilizochukua nafasi ni zile za Ufilipino. 

Naye Mayweather aliwasili katika ukumbi wa MGM Grand Arena na kupokelewa na mamia ya mashabiki wake na baadaye alizungumzia pambano hilo. 

Mpambano huo umekuwa mgumu kutabiri ni nani ataibuka mshindi kutokana na ubora wa mabondia wote wawili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni