Watu wanane ( 8 ) wamefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika eneo la Kipirizi katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma leo.
Taarifa kutoka mkoani humo zinasema kuwa majeruhi wamelazwa kwa matibabu katika hospitali ya mkoa ya Maweni, na baadhi yao tayari wameruhusiwa baada hali zao kuimarika.
Mvua kubwa zilizonyesha leo katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kigoma ziliambatana na radi.
.jpg)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni