Walinzi wawili wameuwawa na watu
kadhaa kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia Chuo Kikuu
cha Garissa leo alfajiri kaskazini mashariki mwa Kenya.
Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya
limesema watu wapatao 30, wakiwemo maafisa polisi wawili wamekimbizwa
hospitali baada ya kujeruhiwa na washambuliaji.
Watu hao wenye silaha inasemekana
wameshambulia taasisi hiyo ya elimu leo majira ya saa 5:30 alfajiri.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni