Mwanamuziki mkongwe wa RnB Billy
Ocean raia wa Uingereza amewasili nchini Uganda tayari kwa ajili ya
kufanya onyesho la muziki liitwalo Black Tie hii leo Jijini Kampala.
Mwanamuziki huyo pamoja na bendi
yake ya watu 16, wamewasili jana na kupokelewa na wenyeji wao kutoka
kampuni ya Master's Music.
Msanii huyo aliyejipatia umarufa
kupitia ngoma za "Caribbean Queen" na "When The Going
Gets Tough," ameahidi kutoa bonge la shoo usiku wa leo Jijini
Kampala.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni