.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Aprili 2015

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA BRAZILI

1 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco Carlos Soares Luz amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015 kuaga.
2
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco Carlos Soares Luz amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015 kuaga.( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu ).

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz na kujadiliana mambo kadhaa kuhusu maendeleo na mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza na Balozi Luz ofisini Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015), Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano ambao ameutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka sita ambacho amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.

Balozi Luz ambaye amepangiwa kwenda Jordan kwenye kituo kipya, alisema anaondoka nchini akiamini kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea mambo aliyoyaanzisha ikiwemo mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao la pamba kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.

Balozi Luz ambaye alifika kumuaga Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili kusomea kozi za Uzamili (Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.

“Wanafunzi hawa wawili waliondoka Februari mwaka huu, ni kati ya wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine watano walikosa ufadhili kutoka kwenye taasisi zao. Mmoja anasomea Geo-Physics na mwingine Oil Engineering,” alisema Balozi Luz.

Balozi Luz ambaye anatarajia kuondoka nchini mapema mwezi ujao, amepangiwa kituo kingine ambapo ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni