Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo la hifadhi lililoombwa kwa ajili ya upanuzi wa manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya waziri wa maliasili na utalii mkoani Iringa leo.
(Picha zote na Loveness Bernard)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akifafanua jambo katika mkutano wa kutatua mgogoro kati ya wawekezaji na wananchi wanaozunguka hifadhi ya Ruaha (mbomipa). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. (Picha zote na Loveness Bernard)
Na Loveness Bernard
SERIKAli imeagiza Jumuia zote za hifadhi za jamii (WMA) nchini kutoingia mikataba na wawekezaji mpaka wanasheria wa wizara ya Maliasili na Utalii kuiidhinisha.
SERIKAli imeagiza Jumuia zote za hifadhi za jamii (WMA) nchini kutoingia mikataba na wawekezaji mpaka wanasheria wa wizara ya Maliasili na Utalii kuiidhinisha.
Akizungumza mjini Iringa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kuwa jumuia hizo zimekuwa zikiingia mikataba ambayo inasababisha wananchi kushindwa kunufaika na rasilimali za maliasili zilizoko katika maeneo yao.
“Migogoro katika hizi jumuia imekuwa mingi karibu nchi nzima, na kwa sasa nadhani imefika wakati kila mikataba lazima iangaliwe na wanasheria katika wizara yangu ili tuweze kujua kama mikataba imekaa sawa”.
Nyalandu ambaye alikuwa mkoani Iringa kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa WMA ya Mbomipa alisema kwamba kwa kipindi kirefu wananchi wa zaidi ya vijiji 20 wilayani Iringa wameshindwa kunufaika na rasilimali hizo.
‘’Wananchi waishio katika vijiji zaidi ya 20 Iringa hawajanufaika na rasilimali zilizoko katika hifadhi ya Ruaha kutokana na mfumo ambao haujawa rahisi kwa watumiaji wa WMA wote nchini , wizara wameamua kurekebisha ili waweze kuepuka migogoro kama hiyo na mikataba yote itakaguliwa na wizara’’
Aidha waziri huyo amekubali ombi la manispaa ya Iringa la kuongeza eneo la iliyokuwa hifadhi ya taifa ya Kihesa kilolo kuwa eneo la Manispaa hiyo kwa jili ya upanuzi wa mji wa Iringa.
Ombi hilo lilitolewa na Manispaa ya Iringa ikiwa ni ombi la kutaka kubadilisha matumizi ya eneo hilo lililokuwa hifadhi kuw amakazi ya watu kwa ajili ya upanuzi wa mji ombo walilotoa kupitia kwa Waziri wa Ardhi Willia Lukuvi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni