Nchi ya Afrika Kusini imewarudisha
kwao raia 400 wa Msumbiji, wiki moja tu kupita baada ya kutokea kwa
machafuko ya kuwashambulia raia wa kigeni katika miji ya Durban
pamoja na Johannesburg yaliyoacha watu kadhaa wakifa.
Hatua hiyo imefuatia operesheni ya
jeshi la polisi iliyobaini mamia ya wahamiaji wanaoishi bila nyaraka
za kuhalalisha uwepo wao nchini Afrika Kusini.
Wengi wa raia wa Afrika Kusini wasio
na ajira wamekuwa wanawalalamikia wageni kwa kuchukua ajira zao
katika nchi yao ambayo ukosefu wa ajira umefikia kiwango cha asilimia
24.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni