Polisi nchini Marekani katika jimbo
la Texas wamesema watu tisa wameuwawa katika mapambano ya silaha
baina ya makundi mawili ya magenge ya waendesha pikipiki katika mji
wa Waco.
Tukio hilo limetokea katika baa ya
Twin Peaks Sports katika eneo la manunuzi la soko la kati la Texas,
ambapo watu 100 wamekamatwa.
Polisi wamesema watu nane wamekufa
papo hapo na mwingine wa tisa amefariki hospitali, wote wakiwa ni
waenesha pikipiki, ambapo wengine wapatao 18 wamejeruhiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni