Msemaji wa Jeshi la polisi Kenya
George Kinoti amesema maafisa polisi 13, hawajulikani walipo na
wengine wawili wamejeruhiwa baada wapiganaji wa al-Shabaab
kushambulia msafara wa magari yao eneo la Yumbis katika kaunti ya
Garissa.
Maafisa polisi waliofanikiwa
kutoroka katika shambulio hilo lililotokea jana usiku, wamesema
magari manne ya polisi yamechomwa moto na wapiganaji hao.
Maafisa polisi hao walikuwa katika
msafara wa magari manne wakielekea Yumbis, saa chache kupita baada ya
polisi mwenzao kushambuliwa jana mchana na wapiganaji wa al-Shabaab.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni