Watu sita nchini Guinea wametengwa
kwenye chumba cha gereza baada ya kutuhumiwa kuusafirisha mwili wa
ndugu yao aliyekufa kwa kuugua Ebola.
Mamlaka za nchi hiyo zimesema mwili
wa marehemu ulikuwa umekalishwa kwenye teksi, ukiwa umevalishwa
fulana, jinzi na mawani ya jua huku ukiwa kati kati ya watu wawili.
Baada ya siku 21 watu hao
hawakuonyesha dalili ya kuwa na virusi vya Ebola na sasa watashtakiwa
kwa kukiuka sheria za afya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni