Kimbunga cha tornado kimeuwa watu 13
katika mji wa kaksazini mwa Mexico wa mpakani wa Ciudad Acuna.
Mamia ya nyumba zimeharibiwa ama
kuteketea katika mji wa jimbo la Coahuila baada tu ya kukatiza mpaka
kutoka Del Rio, Texas.
Jimbo la Texas la Marekani nalo
limeshuhudia mafuriko, ambapo watu watatu wamekufa na makumi
hawajulikani walipo. Picha za nchini Mexico zinaonyesha magari na
majengo yakiwa yameharibiwa vibaya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni