Shirika la Haki za Binadamu la
Amnesty International limesema nchi ya Qatar imefanya jitihada ndogo
katika kuboresha haki za wafanyakazi wahamiaji, licha ya kutoa ahadi
ya kuboresha haki zao.
Mazingira ya kazi na ya makazi
wanazoishi wafanyakazi wa ujenzi wahamiaji nchini Qatar yamekuwa
yakikosolewa mno.
Shirika la Amnesty linafuatilia haki
za wafanyakazi wahamiaji kuelekea maandalizi ya kombe la dunia mwaka
2022, hata hivyo ni jitihada ndogo mno zimefanywa, na katika maeneo
mengi ya ujenzi haki hazizingatiwi kabisa.
Inakadiriwa kuwa wahamiaji milioni
1.5 wanaofanyakazi Qatar, wengi wakiwa kwenye sekta yenye kukua zaidi
ya ujenzi, iliyochochewa na ujenzi wa mandalizi ya michuano ya kombe
la dunia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni