Mtoto mchanga wa miezi 11
amenusurika kifo katika maporomoko ya ardhi nchini Colombia, ambayo
yameuwa watu wapatao 78.
Mama wa mtoto huyo wa kiume pamoja
na ndugu zake wengine 11 walisombwa na maporomoko hayo katika mji wa
Salgar kaskazini-magharibi mwa mkoa wa Antioquia siku ya jumatatu.
Madaktari wanadhani kuwa mtoto huyo
mchanga aitwae jina la Jhosep Diaz, alinusurika kifo kutokana na
kusombwa na kitanda chake na maporomoko ya ardhi kwa umbali wa zaidi
ya kilimota.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni