Wachezaji wa timu ya soka ya Chelsea wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi kuu England 2014/2015 jana. Timu hiyo imeupamba ubingwa wao kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland.
Mchezaji mkongwe wa Chelsea, Didier Drogba ( aliyekaa chini ) akivishwa crown na wachezaji wenzake pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo, Jose Mourinho baada ya kukabidhiwa kombe la ligi kuu England kwa msimu wa 2014/2015. Ligi hiyo ilifikia ukingoni hapo jana.
AHSANTENI VIJANA WANGU!! Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ( aliyeinua mikono juu ) akifurahia baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu England, ambapo Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland naa baadaye timu hiyo kukabidhiwa kombe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni