.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 25 Mei 2015

MBUNGE WA JIMBO LA MVOMERO MH AMOS MAKALLA AFUNIKA, AVIPA VIKUNDI MBALIMBALI MILIONI KUMI NA MOJA

Mamia ya wananchi waliojitokeza kumpokea mbunge wao, Mh Amos Makalla
 Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla ( kushoto ) akikabidhi msaada wa mabati.
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akiwahutubia maelfu wa wananchi wa jimbo la Mvomero.

Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla jana amehutubia maelfu ya wananchi wa mji mdogo Madizini na vijiji vya jirani, huku akikabidhi Fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa vikundi 12 na mabati 200 yenye thamani ya shilingi milioni Tatu kwa ajili ya lupua Jengo la Tawi la CMM Madizini mabati 100, misikiti wa Lusanga Road mabati 50 na kanisa la Full Salvation Church mabati 50.
 

Akihutubia maelfu ya wananchi hao, aliwaeleza kuwa katika kipindi cha uongozi wake amekuwa ni mdau mkubwa wa kusaidia vikundi, makanisa, misikiti na shughuli nyingi za maendeleo, na amewatahadharisha wanaotamani jimbo la Mvomero wajipime kama wanaweza kwani kwa umati huu na matamko yanayotolewa na Makundi mbalimbali jimboni ni dhahiri wanaotaka jimbo la Mvomero ni sawa na mtu anayesubiri Ndege bandarini.
 

Akikabidhi misaada hiyo, alisema ameamua kujibu barua za maombi ya vikundi vya ujasiriamali vya Vijana na akina mama vya vitongoji Sita vya madizini na vikundi viwili vya kijiji cha kichangani. 

Vikundi vilivyofaidika na msaada huo ni mji mpya,kibaite,mpingoni,Kkkt,
barabarani, madizini B, kiwandani, Gezaulole, kazi kwanza, Vijana mpingoni , ushonaji kichangani na soko la ndizi kila kikundi kilipata shilingi laki tano.
 

Aidha alikabidhi mabati 200 kwa ajili ya kusaidia kupaua Jengo la Tawi la CCM madizini bati 100, Jengo la misikiti wa lusanga road bati 50 na Kanisa la full salvation church bati 50.
 

Alivipongeza vikundi hivyo kwa shughuli wanazozifanya, na akawataka wengine kuiga mfano huo kwani umoja ni ushindi. Aliwahaidi ataendelea kuwaunga Mkono kwani katika kipindi chote cha uongozi wake amesaidia vikundi vingi jimboni.
 

Kuhusu kero ya kucheleweshewa malipo ya miwa na mishahara kwa wakulima na wafanyakazi wa kiwanda cha Mtibwa, Mh Makalla ameeleza hatua alizochukua ikiwemo kuipeleka Kamati ya viongozi wa wafanyakazi na wakulima kuonana na Waziri mkuu, na jambo hilo linashughulikiwa na hata hivyo katika hatua ya awali amewakumbusha ujio wa Waziri wa kilimo na Chakula Steven Wasira atatembelea kiwanda hicho na kuongea na menejimenti ya kiwanda, wafanyakazi, wakulima na wananchi leo jumatatu Mei 25' 2015.
 

Amewaomba wawe watulivu wakati huu ambao ofisi ya Waziri mkuu na wizara ya kilimo ikishughulikia tatizo hilo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni