Jumatatu, 25 Mei 2015
UHAKIKI WA VIKUNDI VYA VIJANA VILIVYOPEWA MSAADA WA MASHINE NA NHC WAFANYIKA MIKOANI
Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma Bw. Itandula Gambalagi (mwenye shati jeupe)akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma Bw. Boniface Michael ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kufyatua matofali yanayofungamana katika Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma Bw. Itandula Gambalangi akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Saada S. Mwaruka ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kufyatua matofali yanayofungamana kupitia ufadhiliwa na NHC wa msaada wa mashine ya kufyatua matofali.
Meneja wa NHC Mkoa wa Morogoro Bi. Veneranda Seifa kitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Walace Karia yautekelezaji wa mradi wa vijana wakutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mkashine waliyopewa msaada na NHC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bw. Mbwana S. Magotta (katikati) akiagana na ujumbe wa NHC baada ya kufanya nao mazungumzo ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana. “Jitegemee Vijana” ni moja ya vikundi vilivyokaguliwa na Timu ya NHC Wilayani Gairo.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya na Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma Bw. Itandula Gambalangi wakikagua kikundi cha Challenge Group kilichopo eneo la Chang’ombe Manispaa ya Dodoma ambacho ni moja ya vikundi vilivyofadhiliwa na NHC mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya na Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma Bw. Itandula Gambalagi wakikagua matofali ya kufungamana yaliyotengenezwa na kikundi cha “Ujenzi Group” cha Halmashauri ya Manispaa wa Dodoma.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akitoa msimamo wa NHC wa kukinyanganya mashine tatu kikundi cha Chomtima kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino baada ya kikundi hicho kukaa na mashine nne kilichofadhiliwa na NHC kwa takriban miezi kumi bila kuzalisha matofali yanayofungamana. Kikundi hicho kimeachiwa mashine moja kwa matazamio ya kujirekebisha. Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alishuhudia kupokonywa mashine kikundi hiki na aliomba kupewa muda kuunda kikundi kingine imara ili kipewe mashine zilizopokonywa na NHC.
Ujumbe wa NHC ambao ulifuatana na Maafisa Vijana Wilayani Kilosa wakiwa katika kikao na kikundi cha vijana cha “Nguvu kazi Kimamba B” mji mdogo wa Kimamba Wilayani Kilosa ambapo kikundi hicho kilipewa mwezi mmoja kujirekebisha baada ya kazi yao yakutengeneza tofali kutoridhisha ujumbe huo uliotembelea vikundi vya vijana Wilayani humo kuvikagua.
Ujumbe wa NHC ukiwaeneo la Mvuhakilometa 92 kutoka Manispaa ya Morogoro kukikagua kikundi cha vijana cha Mvu haki lichopewa msaada wa mashine na NHC ya kutengeneza matofali ya kufungamana. Kikundi hiki kiko katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini na kimesha wauzia wananchi matofali na kuwajengea nyumba.
Ujumbe wa NHC ukiichukua mashine moja iliyotolewa kama msaada kwakikundi cha “Mvomero Youth Group” baada ya kikundi hicho kuifungia stoo mashine hiyo kwamiezi takriban sita tangu walipokabidhiwa na NHC badala ya kuanza kuitumia kujiajiri kupitia utengenezaji wamatofali.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akiikabidhi mashine moja aliyoichukua kutoka kikundi cha Mvomero Youth Group kilichoshindwa kuitumia kikamilifu na kukipatia kikundi cha TurianiYouth Group baada ya kuridhishwa na kazi nzuri za kikundi hicho. Kwa kutumia mashine moja waliyopewa na NHC kikundi hiki cha Turiani kimeweza kuwajengea wananchi nyumba kwa kutumia matofali yakufungamana na kina oda nyingi zilizohitaji uwepo wa mashine za kutosha kukidhi mahitaji hayo ya wananchi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni