Tamko lililotolewa jana May 08' 2015 na Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa, International Criminal Court ( ICC ), Fatou Bensouda limewaonya viongozi wa serikali ya Burundi kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo wakati ikiwa inajiandaa na uchaguzi wake mkuu mwezi wa sita mwaka huu.
Taarifa hiyo imesema ICC inafuatilia kwa ukaribu hali inavyoendelea nchini humo.
Burundi imekumbwa na machafuko ya maandamano mfululizo kutoka kwa wananchi wakipinga Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa kuiongoza Burundi.
Katika machafuko hayo, watu kadhaa wameshapoteza maisha yao, huku wengine kwa mamia wakivuka mipaka kukimbilia nchini Tanzania kutafuta hifadhi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni