Jeshi la Nigeria limesema
limesafisha zaidi ya kambi 10 zilizokuwa zikitumika na kundi la Boko
Haram, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Kumekuwa na mapigano makali karibu
na kambi ya Dure, ambayo taarifa zinaeleza kuwa kambi hiyo ni moja ya
maficho maarufu ya wapiganaji wa Boko Haram.
Kundi la Boko Haram halijatoa kauli
yoyote juu ya taarifa hiyo ya jeshi na pia hakuna chanzo huru
kilichothibitisha taarifa hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni