Muuguzi wa kike nchini India ambaye
ameishi kwa miaka 42 akiwa katika hali ya umahututi baada ya kubakwa
na kukabwa koo amefariki dunia.
Muuguzi huyo Aruna Shanbaug alipatwa
na madhara makubwa ya ubongo na kupooza mwili baada ya shambulio hilo
la kubakwa lililofanywa mwaka 1973, na mhudumu wa wodini katika
hospitali ya Mumbai aliyokuwa akifanyakazi.
Kwa kipindi chote cha miaka 42,
Shanbaung alikuwa analishwa kwa kutumia mpira wa puani, lakini katika
siku sita zilizopita alipatwa na nimonia, na baadae kupoteza maisha.
Tukio lake liliibua mjadala mzito wa
kisheria mahakamani, na mahakama ya juu ya India ilikataa ombi la
kuruhusu aondolewe uhai.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni