Mafundi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa jengo jipya katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Uongozi wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika ujenzi unaoendelea wa jengo la kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyere (JNIA).
Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu za abiria kupandia na kushuka kwenye ndege, ofisi za uhamiaji na huduma zingine muhimu.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Suleiman S. Suleiman amesema kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hapo awali kilikuwa na uwezo wa kuruhusu ndege sita tu kutua kwa saa lakini kwa sasa unaweza kuruhusu ndege hadi 30. Tunatarajia kuongeza ndege zaidi na hivyo kuufanya kiwanja hiki kuhimili 2500 tofauti na abira 700 wa awali pindi ujenzi huu utakamilaka.
Kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 85, katika awamu ya kwanza ambayo inategemewa kukamilika Juni mwaka 2016 na itakiwezesha JNIA kuhudumia abiria milioni tatu na nusu kwa mwaka. Iwapo ujenzi wa awamu ya pili utakamilika mwaka 2017 JNIA kitakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria milioni sita kwa mwaka.
Alipokuwa akitembelea mradi huo, Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri, aliuambia uongozi wa Mamlaka hiyo kuzingatia wazo la kuwa na huduma zote za msingi katika kiwanja cha Julius Nyerere ili kuweza kushindana viwanja vya nchi jirani na barani Afrika kwa ujumla.
“Ni vema kuwa kiwanja chetu cha ndege kinapanuliwa ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi, lakini nimegundua kuna vitu muhimu vimesahaulika katika usanifu wa upanuzi huu, kuna vitu kama hoteli, jengo la hospitali, sehemu za kupata huduma za kibenki na pia namna nzuri ya kuwapatia abiria watuao usafiri wa kwenda mjini na sehemu nyinginezo, nadhani haya pia yazingatiwe, alisema Bibi. Mwanri.
Uwepo wa huduma hizi utawavutia abiria kutumia kiwanja chetu kuliko vya majira zetu na pia kutakuza mapto ya TAA na taifa kwa ujumla.
Ujenzi huu unaoendelea umezingatia haja ya kuunganisha majengo yote matatu ili kurahisisha uunganishaji wa ndege za ndani na za nje pia upokeaji wa mizigo.
Serikali kupitia Tume ya Mipango, imeshaanza kuandaa Mpango wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 wenye dhima ya kukuza uchumi wa kiviwanda hivyo basi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inapaswa kuwa chachu ya mpango huu kwa kusafirisha watu na bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo”alisema Bibi. Mwanri.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni