.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Mei 2015

JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LINAWASHIKILIA WATU 37 KWA KOSA LA KUFANYA FUJO

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu 37 kwa kosa la kufanya fujo kwa kuzuia watu wengine kutoa huduma ya usafiri kama Bajaji na magari ya watu binafsi kwa kuwapiga watu wanaopanda vyombo hivyo vya usafiri, kupiga magari kwa mawe na kufunga barabara.

Watu hao wamekamatwa kwenye mitaa ya Nkuhungu katika barabara ya kwenda Singida na Chadulu kwenye barabara ya Morogoro katika Manispaa ya Dodoma.

Akifafanua kuhusu kukamatwa kwa watu hao 37 amesema ni wale tu waliokwenda mbali zaidi na kujichukulia sheria mikononi, ila kwa wale wote walioegesha magari yao kwenye vituo au pembezoni mwa barabara hawakukamatwa.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime ametoa wito kwa watu wote kwamba ni marufuku watu kuzuia wengine kutoa huduma, ni marufuku watu kuharibu mali za wengine. Wanaofanya uharifu huo watakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni