Na Lorietha Laurence-Maelezo
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ameishauri kamati ya maandalizi ya Tuzo ya Tanzania Film Awards kuhakikisha kuwa wanaitanganza tasnia ya filamu kimataifa.
Akiongea na kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha kupokea taarifa ya Maandalizi ya Tuzo hizo kilichofanyika katika ukumbi wa wizara ambapo aliwapongeza viongozi wa kamati hiyo kwa juhudi walizozifanya.
“kazi mnayoifanya ni nzuri kwa kuwa inasaidia kukuza na kuitangaza tasinia ya filamu na hivyo kuwavutia wadau mbalimbali kuwekeza zaidi” alisema Prof.Elisante.
Aidha amewataka viongozi wa kamati hiyo kuhakikisha kuwa tuzo zitakazotolewa siku hiyo ziwe za ubora na kiwango cha juu ili kuwahamasisha waandaji wa filamu kuandaa filamu zenye viwango vizuri zaidi.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Tuzo hizo Bibi. Caroline Gul ameeleza kuwa mpaka sasa wamefanikiwa katika maandalizi mbalimbali ikiwemo ukumbi,tuzo zitakazotolewa na amajaji.
“Mpaka sasa tumefanikisha katika suala la ukumbi na kupokea filamu 300 ambazo zipo katika vipengele 12 zenye jumla ya washiriki 50 watakaoshindanishwa siku hiyo” alisema Bibi. Caroline.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fisoo ameishukuru kamati hiyo kuweza kushirikiana na Serikali kwa kila hatua wanayoifanya katika maandalizi ya tuzo hizo.
“Serikali inatambua mchango wenu katika kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu nchini ni jambo zuri kwa kuwa inasaidia kukuza soko la tasnia hii kimataifa” alisema Bi.Fisoo.
Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia nia Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Saimon Mwakifwamba ameeleza kuwa wamefanikiwa kualika majaji kutoka East Africa Film Network ambao watasaidiana na majiaji wa hapa nchini katika kupata washindi.
Tuzo za Tanzania Film Awards zinatarajiwa kufanyika tarehe 23 May katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambapo tikite zitauzwa kuanzia elfu 50 mpaka laki moja kwa VIP.
Tuzo za Tanzania Film Awards zinatarajiwa kufanyika tarehe 23 May katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambapo tikite zitauzwa kuanzia elfu 50 mpaka laki moja kwa VIP.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni