Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). (Picha zote na Zainul Mzige).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimweleza yaliyomo kwenye taarifa ya ripoti ya hali ya Elimu ilivyo dunia (EFA Global Monitoring Report 2015) “Education For All 2000-2015” ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto kidunia iliyoandaliwa na Shirika la UNESCO alipomtembelea ofisini kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja mjini Dodoma ambapo pia alikutana na wadau wa sekta ya elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Elimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akimwonyesha takwimu za Tanzania zilizomo kwenye ripoti hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO, Zulmira Rodrigues (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma.Na Modewjiblog team
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa
(TAMISEMI), Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi
katika kumwezesha mtu kujitegemea.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog
kuhusu maendeleo na changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki
ya maadhimisho ya elimu inayofikia tamati leo mjini Dodoma.
Alisema
katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa unawaondoa watu kwenye ajira
ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji wa elimu ndio kitu cha
msingi kabisa.
Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini.
Alisema
kuna mambo mengi ambayo yanastahili kuangaliwa kwa sasa kutokana na
vigezo vya ufanisi wa elimu kuonesha changamoto zinazokabili sekta hiyo
pamoja na kuimarika kwake.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupungua kwa uandikishaji wa watoto na mdondoko.
Alisema
viongozi, wazazi pamoja na walezi wamesahau wajibu wao na kumwachia
mwalimu pekee katika kumlea mwanafunzi kimasomo na hii ndio chanzo
kikubwa cha mdondoko na ufaulu mbaya.
Alisema ni vyema watu wakajiuliza hawa wanaondoka wanakwenda wapi na wanafanya nini.
“kuna
sheria ambapo viongozi wa kata wanaruhusiwa kuwachukulia hatua na
kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokwamisha elimu, lakini watu
hawachukia sheria hiyo” alisema.
Aidha alisema ubora wa elimu
una vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kujituma kwa walimu katika
ufundishaji na kuwa na dhamira ya kuwapa watoto vitu vyenye maana.
Alisema
kuna mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuinua elimu na usimamizi
unapokuwa mkali na wahusika kuadhibiwa ndio ufanisi unafanyika na
mdondoko kuangaliwa.
Alisema ipo haja kubwa ya kuwekeza kwenye elimu kwa viongozi na wadau kutimiza wajibu wao.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi , Makuru Petro akitoa tathmini ya sekta ya elimu kwa
wadau wa sekta ya elimu alisema pamoja na ongezeko la ufaulu ndani ya
miaka miwili ipo haja ya kutathimini uimara wa mfumo katika kutoa huduma
ya elimu.
Alisema pamoja na ufanisi kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wanaokacha shule kunaonesha mfumo kuwa na kasoro na lazima uangaliwe.
Aidha
alisema sekta ya elimu wamepokea asilimia 97 ya bajeti yake na kwamba
asilimia 70 imeenda kwenye halmashauri ambako ni watekelezaji wa miradi
ya elimu.
Tathmini hiyo inayowakilisha wizara zote
zinazoshughulikia elimu kama TAMISEMI, Elimu na Maendeleo ya jamii na
wadau wengine wa elimu ni sehemu ya shughuli inafanywa kila mwaka kwa
lengo la kutambua kilichofanyika, changamoto na namna ya kukabiliana na
tatizo hilo.
Hata hivyo walisema kwamba ndani ya miaka miwili
kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu hasa ufaulu na
ubora wa elimu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni