.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 15 Mei 2015

BAADHI YA VIONGOZI WA JARIBIO LA MAPINDUZI BURUNDI WAKAMATWA

Kunataarifa zinaeeleza kuwa baadhi ya viongozi wa jaribio la kuipindua nchi ya Burundi lililoshindikana wamekamatwa.

Haijafahamika mara moja iwapo Jenerali Godefroid Niyombare, aliyetangaza mapinduzi ni miongoni mwa watu waliokamatwa.

Mmoja wa jenerali msaliti aliyejaribu kutwaa madaraka nchini Burundi amesema anamini jaribio lao la kutaka kumng'oa madarakani rais Pierre Nkurunziza limeshindikana.

Jenerali Cyrille Ndayirukiye ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa wengi wa wanajeshi wanataka serikali ya sasa iendelee kuwepo madarakani.

Wakati huo huo, rais wa Nkurunziza ametwiti katika ukurasa wake wa twitta kuwa amerejea nchini Burundi, na kunataarifa kuwa sauti yake imesikika katika redio ya taifa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni