.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 2 Mei 2015

LIGI KUU UINGEREZA, STEVEN GERALD ACHANGIA USHINDI WA LIVERPOOL KUIFUNGA QPR 2-1

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerald amefunga bao kunako dakika za majeruhi na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Qeens Park Rangers ( QPR ) katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliochezwa leo.
Wakicheza nyumbani, Liverpool ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Philippe Coutinho katika dakika ya 19, bao ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili wageni QPR walisawazisha bao hilo katika dakika ya 73 mfungaji akiwa ni Leroy Fer, hata hivyo Gerrard akaipatia Liverpool bao la ushindi katika dakika ya 87.
Kwa matokeo hayo, Liverpool wamefikisha pointi 61 wakiendelea kubaki katika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni