Mahakama nchini Misri imemuhukumu
adhabu ya kifo rais aliyeng'olewa madarakani Mohammed Morsi, kutokana
na tukio la kuvunjwa gereza na kutoroka wafungwa wengi mwaka 2011.
Kiongozi huyo wa zamani
alishahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuagiza kukamatwa na
kufanyiwa mateso waandamanaji waliokuwa wanaupinga utawala wake.
Kwa sasa chombo cha kidini chenye
mamlaka nchini Misri, kinasubiriwa kutoa maoni yao kabla ya hukumu
hiyo ya kifo kutekelezwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni