Mahakama nchini Marekani imemuhukumu
adhabu ya kifo kwa kuchomwa sindano Dzhokhar Tsarnaev aliyehusika na
tukio la milipuko ya bomu iliyotokea Boston.
Watu watatu waliuwawa katika tukio
hilo na wengine 260 walijeruhiwa wakati Tsarnaev na kaka yake
walipoweka milipuko ya mabomu katika eneo la kumalizia mbio za
Marathoni za Boston mwaka 2013.
Inawezekana sasa Tsarnaev akapelekwa
kwenye gereza la Terre Haute, Indiana, angingojea kutekelezewa adhabu
hiyo, lakini kunauwezekano pia kukawa na hatua ya kukata rufaa katika
mahakama za juu.
Waathirika wa tukio hilo walitokwa
na machozi wakati hukumu hiyo ikisomwa lakini Tsarnaev hakuonyesha
hisia zozote.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni