Mahakama nchini India imesitisha
adhabu ya kifungo aliyopatiwa muigizaji filamu nyota Salman Khan,
ambaye ametiwa hatiani kwa mauaji mwaka 2002, katika tukio la kesi ya
kugonga watu na kukimbia, wakati huu pingamizi lake likisikilizwa.
Jumatano ya wiki hii mahakama ya
Mumbai ilimuhukumu Khan kwenda jela miaka mitano, kwa kumua Noor
Ullah Khan kwa kumgonga na gari wakati akiwa amelala kando ya
barabara.
Mahakama Kuu ya Bombay ilimpatia
dhamana ya muda kwa siku mbili, baada wakili wake kuwasilisha
pingamizi la hukumu hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni