Majenerali wa Jeshi la Burundi
wamempindua rais Pierre Nkuruzinza, huku taifa hilo likiendelea kuwa
na machafuko kutokana na uamuzi wake wa kutaka kuwania urais kwa
muhula wa tatu.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh
amesema kamati ya taifa ya kulikomboa taifa hilo imeundwa ili
kuiongoza nchi hiyo.
Hata hivyo haijafahamika mara moja
iwapo Meja Jenerali Niyombraeh anaungwa mkono kwa kiasi gani na
maafisa wengine wa jeshi.
Rais Nkuruzinza ambaye yupo nchini
Tanzania ingawa hajaonekana katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki unaojadili mgogoro wa nchi yake. Msaidizi wake ameelezea
mapinduzi hayo kuwa ni mzaha.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni