Mkurugenzi wa kupunguza umaskini kutoka Wizara ya Fedha, Ana Mwasha (kulia) akifungua kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano na Katikati ni Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama.( Picha na Zainul Mzige )
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akizungumza kwenye kongamano la siku moja linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF).
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano akizungumza kwenye kongamano hilo.
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
Dk. Kenneth Mdadila kutoka kitengo cha uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano hilo.
Pichani juu na chini baadhi ya wadau walioshiriki kwenye kongamano hilo wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Alisema
mahitaji ya msingi katika kupunguza umasikini, hayajafikiwa kwani
tumefikia asilimia 28.2 wakati tulitakiwa kuwa asilimia 19.
Alisema ipo haja kubwa ya kuangalia utekelezaji wa malengo endelevu kwa kuoanisha na mikakati mingine ya kidunia na ya kikanda, huku kazi kubwa ikiwa kuhakikisha malengo yote 17 yanatekelezwa katika muda uliopangwa.
Katika kongamano hilo, washiriki walipata nafasi ya kumsikia Balozi Celestine Mushy kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akichambua jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo anafikiri Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
Pia katika majadiliano, washiriki waliozungumzia haja ya kuangalia takwimu kwa kuoanisha kwani zimekuwa zikitafutwa na kila mtu mpaka hazijulikani nani yuko sahihi.
Aidha, walitaka mkakati wa kiviwanda ndio uzingatiwe kwani ndio unaoonesha dira ya kufanikisha maendeleo ya kitaifa, kikanda na kibara.
Kongamano hilo liliendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi (ESRF) kwa ufadhili wa UNDP.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni