.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 31 Mei 2015

MBUNGE WA MVOMERO, MH AMOS MAKALLA AZIDI KUTOA MISAADA MBALIMBALI KWA WANANCHI WAKE

 Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla akiwahutubia wananchi waliofurika katika mkutano wake.
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wakimshangilia mbunge wao, Mh Amos Makalla ambaye wamekiri kuwa amefanya mambo mengi jimboni humo.
 Mh Amos Makalla akiwahutubia wananchi waliofika katika mkutano wake.
Mbunge wa Mvomero, Mh Amos Makalla akikabidhi fedha taslimu kwa vikundi mbalimbali vilivyopo jimboni mwake.
Mamia ya wananchi wakimpokea kwa furaha mbunge wao, Mh Amos Makalla. 

Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla amezidi kukonga nyayo za wananchi wa Mvomero kwa kuendelea kusaidia misaada mingi ya maendeleo jimboni kwake, na  leo akihutubia mamia ya wananchi katika kijiji cha Kidudwe.

Mh Makalla ametoa msaada kwa vikundi vitano vya ujasiriamali,misaada aliyotoa Mh Makalla ni pamoja na mabati kwa ajili ya msikiti wa sekondari ya Mtibwa, Kanisa la Kibaptisti, computer mbili na printer kwa ajili ya Saccos ya walimu Mvomero na nyingine kwa ajili ya Saccos ya vijana wilaya Mvomero, misaada yote ikiwa na thamani ya shilingi milioni nane.
 

Akikabidhi misaada hiyo, mbunge wa Mvomero aliwaeleza kuwa kwa miaka mitano imekuwa utamaduni wake kusaidia wananchi wake na amefanya hivyo kwa vikundi vingi na alisema amekabidhi misaada hiyo ikiwa ni kujibu barua za maombi alizozipata  kupitia vikundi na taasisi mbalimbali.
 

Aliwashukuru sana viongozi wa vikundi kwa kujiunga katika vikundi, kwani kuna rahishisha utendaji kazi na hivyo ni vizuri kusaidia vikundi kuliko kumsaidia mtu mmoja.
 

Viongozi wa vikundi, madhehebu ya dini na Saccos kwa pamoja wamemshukuru mbunge wao kwa utendaji wake mzuri wa kazi na misaada mingi anayoitoa kwa wananchi, kwani hii inaonyesha namna ambavyo mbunge wetu anavyowajali wananchi, walisema.
 

Aidha amewahakikishia kuwa tatizo la Maji na Umeme kwa kijiji cha kidudwe litakwisha hivi karibuni, kwani wananchi wanaona jitihada anazozifanya na  mkandarasi wa Maji yupo kazini na wa Umeme atakuwepo kazini wiki ijayo.
 

Amewataka wananchi kuwapa ushirikiano wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Maji na Umeme ili wakandarasi watekeleza miradi hiyo kwa kasi na ufanisi zaidi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni