Takwimu zilizotolewa na gazeti la
Washington Post zinaeleza kuwa idadi ya watu waliopigwa risasi na
maafisa polisi wa Marekani ni mara mbili zaidi kuliko takwimu rasmi
zilizotolewa.
Gazeti hilo limesema katika miaka
mitano ya kwanza ya mwaka huu watu 385 waliuwawa kwa kupigwa risasi
na polisi, ikiwa ni zaidi ya watu wawili kuuwawa kwa kila siku.
Katika takwimu hizo idadi ya
Wamarekani weusi waliouwawa ilikuwa ni kubwa na wengi wakiuwawa bila
ya kuwa na silaha yoyote inayoweza kutishia usalama wa polisi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni