Benki mbili za Ulaya zimeanza
kupitia nyaraka zake ili kubaini kama zilitumika kufanya malipo ya
rushwa kwa maafisa wa Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa).
Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI)
siku ya jumatano lilielezea kuhusika kwa mabenki ya Standard
Chartered, Barclays pamoja na HSBC, na kesi inayowakabilia maafisa 14
wa Fifa waliokamatwa nchini Uswizi.
Benki ya Barclays na HSBC zimekataa
kuzungumzia suala hilo huku benki ya Standard Chartered ikisema
inachunguza malipo hayo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni