Mshauri wa serikali ya Libya amesema
wasafirishaji watu kwa njia za magendo wamekuwa wakiwasafirisha
wapiganaji wa kundi la Dola ya Kiislam (IS) kupitia bahari ya
Mediterranean.
Msemaji huyo Bw. Abdul Basit Haroun
amesema wasafirishaji hao huwaficha wapiganaji wa kundi la IS kwenye
boti zilizojaa wahamiaji haramu.
Maafisa wa taifa la Italia na Misri
walishatoa tahadhari kwamba wapiganaji wa IS, wanaweza kufika bara la
Ulaya kwa kutumia boti za wahamiaji haramu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni