Mamlaka nchini Misri leo imewanyonga
wanaume sita waliotiwa hatiani kwa kuwauwa wanajeshi, licha ya kuwepo
kwa pingamizi linalodai kuwa wawili miongoni mwa hao walikuwa
kizuizini wakati mauaji hayo yakitokea.
Mahakama ya jeshi ilikazia hukumu
yao mwezi Machi, kufuatia kutiwa hatiani kwa watu hao sita katika
kesi inayohusu kufanya mashambulizi baada ya jeshi kumg'oa madarakani
rais Mohammed Morsi Julai 2013.
Waendesha mashtaka walisema
watuhumiwa hao sita walikuwa ni wafuasi wa kundi la jihadi la Ansar
Beit al-Maqdis lenye maskani yake katika eneo la Sinai, kundi ambalo
limetangaza kushirikiana na Dola ya Kiislam (IS).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni