Watu wapatao watatu wamekufa
kufuatia shambulio la bomu la kujitoa muhanga karibu na eneo la
kuingilia uwanja wa ndege wa Kimataifa Jijini Kabul nchini
Afghanistan.
Shambulio hilo limefanywa karibu na
eneo linalotumiwa kuegesha magari ya wanajeshi, na pia lililenga gari
la mafunzo ya polisi la vikosi vya Ulaya.
Mtu mmoja aliyekuwa ndani ya gari
alikufa pamoja na watoto wawili wa kike wa Afghan, ambapo pia watu
wapatao 20 wamejeruhiwa. Kundi la Taliban limekiri kufanya shambulio
hio.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni