Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani,
Papa Francis amewatangaza masita wawili walioishi karne ya 19, wakati
wa utawala wa Ottoman nchini Palestina kuwa ni watakatifu. Masista
hao wanakuwa watakatifu wa kwanza waliokuwa wakiongea lugha ya
kiarabu.
Watakatifu hao Marie Alphonsine
Ghattas pamoja na Mariam Bawardy ni miongoni ya watakatifu wanne
wapya waliotangazwa Jijini Rome katika eneo la St Peter's Square.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas
pamoja na mahujaji wa kikristo zaidi ya 2,000 kutoka ukanda huo
wamehudhuria sherehe hizo.
Uamuzi huo unaonekana kuwa ni ishara
ya Vatican kuwaunga mkono wakristo wanaoishi katika mazingira ya hofu
katika mataifa ya Mashariki ya Kati.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni