Timu ya Paris St Germain imekuwa
mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa kwa mara ya tatu mfululizo, huku
ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya jana kuifunga Montpellier kwa
mabao 2-1.
Timu hiyo inayomilikiwa na Qatari
ilikuwa inahitaji pointi moja tu ili kutangazwa msshindi lakini
ikapata pointi tatu na kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane,
dhidi ya Lyon iliyotoa sare ya 1-1 dhidi ya Girondins Bordeaux.
Wachezaji wa Paris St Germain wakishangilia ushindi kwa kucheza
Kocha wa Paris St Germain Laurent Blanc akifurahia ushindi na Matuidi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni