Mwanamke mwenye umri wa miaka 65
nchini Ujerumani amejifungua watoto watatu baada ya kutunga mimba kwa
njia za kupandikiza kisayansi.
Kituo cha runinga cha RTL nchini
Ujerumani kimesema mwanamke huyo Annegret Raunigk, amejifungua watoto
wawili wa kiume na mmoja wa kike kwa njia ya upasuaji Jijini Berlin.
Watoto hao wamezaliwa kabla ya muda
wao wakiwa na wiki 26, hata hivyo madaktari wamesema wote wapo katika
hali nzuri ya kuweza kuishi.
Annegret Raunigk ambaye alikuwa na
watoto 13 pamoja na wajukuu saba, ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa
kwanza duniani mwenye umri mkubwa kujifungua mapacha watatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni