Umoja wa Mataifa umesema wakimbizi
wa Burundi 3,000 wanaugua kipindupindu nchini Tanzania, katika Mkoa
wa Kigoma ambao wakimbizi hao wamekimbilia kuepuka machafuko nchini
kwao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi limesema kila siku wagonjwa 400 wapya
hujitokeza.
Zaidi ya wakimbizi 100, 000
wamekimbia Burundi katika wiki za hivi karibuni wakikimbia vurugu
zilizochochewa na hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania
urais kwa muhula wa tatu.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni