Wafungwa watatu hatari wametoroka
kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Kamiti nchini Kenya usiku wa jana
tukio ambalo lilipelekea kupigwa risasi kimakosa mwanamke mmoja
wakati askari magereza wakijaribu kuwatafuta wafungwa hao.
Maafisa wa magereza Kenya wamesema
tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wakati ambapo wafungwa
hao walipokata nondo za chuma kwenye chumba chao na kisha kutoroka.
Kwa mujibu wa OCPD wa Kasarani
Francis Sang, baada ya kitendo hicho alamu ililia na ndipo askari
waliposhtuka na kuwafuatilia wafungwa hao huku wakifyatua risasi
ambapo mwanamke mmoja alipigwa risasi kwa bahati mbaya na kujeruhiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni