Mwanariadha Usain Bolt ameshinda
kirahisi mbio zake za kwanza Ulaya, lakini ameshindwa kuvunja rekodi
yake ya kutumia sekunde 20 katika mbio za mita 200 za Golden Spike
huko Ostrava.
Mbio hizo kwenye mazingira baridi
Mjamaica huyo aliyetwaa medali sita za dhahabu za katika michuano ya
Olimpiki, alitumia sekunde 20.13, na kushindwa kufikia rekodi yake ya
dunia ya sekunde 19.19
Akiongea baada ya mbio hizo Bolt
anayejianda na mbio za mabingwa wa dunia za Bejing amesema
hajaridhika kutokana na kushindwa kushinda chini ya sekunde 20.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni