Maafisa waandamizi wa Shirikisho la
Soka Duniani (FIFA) pamoja na maafisa wa soko wamekamatwa leo asubuhi
na polisi wa nchini Uswizi kufuatia mashtaka ya rushwa yaliyotolewa
na Marekani.
Maafisa hao ambao ni sehemu ya vyama
wa kimataifa vya soko, wanatarajiwa kurudishwa Marekani baada ya
kukamatwa kwenye hoteli moja ya kitalii nchini Uswizi.
Zaidi ya maafisa 10 wa Fifa
wanatarajia kufunguliwa mashtaka kwa kuhusika na uhalifu,
utakatishaji fedha haramu Jijini New York na Idara ya Sheria ya
Marekani.
Mashtaka hayo ni changamoto kubwa
kwa Fifa, ambayo rais wake Sepp Blatter anatafuta nafasi ya kuwania
muhula wa tano katika uchaguzi utakaofanyika Ijumaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni